Ingawa kuongezeka kwa vituo vya redio vinavyotumia lugha ya Kiswahili kwenye maeneo ya Afrika Mashariki kulitazamiwa kuwe neema kwa lugha hiyo, wasomi na wataalamu wa lugha wanahofia kwamba aina ya Kiswahili kinachotumiwa kwenye vituo hivyo vya redio kinakwamisha maendeleo halisi ya Kiswahili. Msikilize hapa Profesa Ken Walibora akizungumzia mashaka aliyonayo juu ya namna Kiswahili “kinavyopotoshwa” kwenye vituo vya redio za FM nchini Kenya na Tanzania.