KISWAHILI KINA WENYEWE

Fasihi ya Kiswahili katika zama za TEHAMA

Wakati teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ikizidi kuimarika na kuchukua nafasi ya njia kongwe za mawasiliano, fasihi ya Kiswahili nayo inajikuta kwenye changamoto ya kuakisi mabadiliko hayo ya kiwakati.

Dk. Aldin Mutembei wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (TATAKI) anazungumzia nafasi ya fasihi ya Kiswahili kwenye zama hizi mpya za mawasiliano, ambapo mitandao ya kijamii imekuwa jukwaa kubwa kabisa la mawasiliano.

Kwa mujibu wa Dk. Mutembei, fasihi ya Kiswahili haijapitwa na kasi ya teknolojia mpya na badala yake imekuwa ikienda sambamba na mageuzi kwenye jukwaa hili la mawasiliano. Hata hivyo, mtaalamu huyo wa fasihi anakiri kwamba kuna changamoto kadhaa ambazo wanafasihi wa Kiswahili wanapaswa kukabiliana nazo ili uasili wa fasihi ya Kiswahili isipotee.

Bonyeza hapa kumsikiliza mtaalamu huyu wa Kiswahili.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.