Mbazi chakula gani, mgeni kukirimiwa?
Nazitoke ugenini, nchini zikaingia
Zikainjikwa jikoni, kachanua kama ua
Zikaweka mezani, zikafunikwa na kawa
Ukaalikwa mgeni, sahani ukajaziwa
Hunabudi mgeni, kula moja kama dawa
Mbaazi chakula gani, mgeni kukirimiwa?
Wanaopenda mbaazi, hii ni hasara yao
Japo ni kitu azizi, kwa sifa na mila zao
Sitajitia ajizi, hashiriki mwendo wao
Kwangu kuzila mbaazi, sawa kuwa na wao
Mungu sinipe mapenzi yakufata mwendo wao
Siwezi katu siwezi, naogopa watu hao
Mbaazi chakula gani mgeni kukirimiwa?
Chakula hiki jamani, hadi uchotee upawa
Kinanipa kisirani, wakila bila kunawa
Walaji wake jamani, ukiwaona ‘tajuwa
Akizaliwa kwetu ndani, au mgeni ikawa
Kingine hawakioni, chakula wakavutiwa
Mbaazi kwao mbaazi, ndicho wanachojuwa
Mbaazi chakula gani, mgeni kukirimiwa?
Said Miraaj Abdulla
Dar es Salaam