KISWAHILI KINA WENYEWE

Hisabati ya Kiswahili: Baina ya uambishaji na unyambulishaji

Uambishaji ni dhana inayowakilisha upachikaji wa vipashio vya kisarufi kwenye mzizi wa neno kwa minajili ya kujenga ama neno jipya au kubadilisha tu hali ya neno.

Kwa mfano, mzizi wa neno -pig- ukiwekewa viambishi ku-pig-a unakuwa kitenzi au kitenzi nomino na ukiwekewa pig-o unakuwa nomino. Inaweza kuwa u-pig-aji, ma-pig-ano, m-pig-aji na kadhalika.

Kuna utata wa kitaalamu juu ya ikiwa Kiswahili kina aina tatu za viambishi – yaani awali, kati na tamati – au kina aina mbili tu – yaani awali na tamati. Hoja zote mbili zina nafasi yake katika taaluma ya lugha na haziondowi ukweli kwamba Kiswahili kinaambisha.

Kwa upande mwengine, unyumbuaji ni kuvipachua hivyo vipashio vilivyounganishwa kwenye neno moja na kuvipa tafsiri yake ya kisarufi. Kwa mfano, neno (au sentensi) “Ninakuona” inaweza kunyumbuliwa hivi ifuatavyo:

i. Ni-: kiambishi awali cha nafsi ya kwanza umoja, yaani mimi, katika hali ya utendaji
ii. -na-: kiambishi awali kinachowakilisha wakati uliopo
iii. -ku-: kiambishi awali kinachowakisha nafsi ya pili, umoja, yaani wewe, katika hali ya utendwaji
iv. -on-: mzizi wa neno wa kitenzi ona
v. -a: kiambishi tamati kinachowakilisha hali ya utendaji

Kwa hivyo, kwa muhtasari uambishaji ni upachikaji vipashio vya kisarufi kwenye mzizi wa neno na unyumbulishaji au unyumbuaji ni upachuwaji wa vipashio hivyo na kuvichambua kisarufi.

Ni hayo kwa sasa. Je, una mifano au maoni zaidi juu ya uambishaji na unyambulishaji? Karibu tukisemee Kiswahili.

13 thoughts on “Hisabati ya Kiswahili: Baina ya uambishaji na unyambulishaji”

  1. mm kwa upeo wangu mdogo nafahamu uambishaji(inflaction) kuwa ni upachikaji wa viambishi ktk mzizi ambao una sababisha mabadiliko ya kisarufi kama hali umoja ya wingi , njeo n.k.kwa mfano: m-tu na wa-tu.a-na-som-a. hivyo uambishaji haubadili kategoria ya neno.

    1. Upeo wako si mdogo hata kidogo Ulfat. Tunataraji ndivyo pia uchambuzi huu ulivyosema. Ingawa la ikiwa uambishaji unaweza kubadili kundi la meno (kategoria kwa kutumia utohoaji wako), tunaamini kuwa uambishaji hufanya hivyo, yaani huweza kuliondoa meno kutoka kundi moja ya neno (kama vile zuri ambayo ni kivumishi) na kuw aina nyengine ya neno (kama vile uzuri ambayo ni nomino). Ahsante sana.

  2. Je, Unyambulishaji ni kupachika viambishi tamati peke yake au pamoja na viambishi awali?
    Dhana ya mnyumbuliko bado haijakaa vizuri

  3. Nashukuru kwa mtoa mada.
    Mimi sijakuelewa unapotoa fasili ya unyumbulishaji kuwa nikitendo cha kupachuwa viambishi. ukiwa na maana ya kufafanua kiambishi na kazi yake .kwa uelewa wangu , nsfahamu kuwa
    UNYAMBULISHAJI ni kitendo cha kupachika viambishi mwishoni mwa mzizi wa neno au shina LA neno.

    MF. chez- cheza, chezea, chezesha
    safi- safisha , safika, safishika, safishana n.k.

    mfano wa kwanza nimetumia mzizi.
    MF 2 nimetumia shina

  4. Mtoa mada kiukweli anapaswa kwenda kuangalia namna wanaisimu nbalimbali kama akina prof massamba, akna mgullu na kina Kindija wanavyozitazama dhana hizo

  5. Ni sawa kabisa jinsi wenzangu walivyojaribu kusema kuhusu uambishaji na unyambuaji lakini bado kuna utata ambao watalaamu Wa lugha into wanafaa kutafiti zaidi

  6. Dhana ya mnyambuliko ni dhana zelezi kwa wanaisimu wengi

    nijuavyo kutokana na chambuzi za wanaisimu wengi ni kwamba DHANA KUU NI

    MNYAMBULIKO/UNYAMBUAJI ambao ni kitendo cha kupachika viambishi kwenze mzizi wa neno

    Aina zake ni

    1. Uambishaji…kitendo cha kupachika viambishi kabla ya mzizi mfano a-na-vyo-lima

    2. Unyumbuaji….kitendo cha kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno mfano Lim-i-a

  7. Unyumbulishaji limetokana na neno “Nyumba” likiwa na maana ya kawaida ya kurefusha neno.

    Hivyo katika sarufi ya kiswahili Unyumbulishaji maana yake ni kitendo cha kurefusha neno (kupata misamiati tofauti katika neno) Kwa kutumia viambishi tamati. (Danstani Mgouya)

  8. Aksante mtoa mada, mimi ninavyofahamu kwa hayo ni kuwa unyambuaji ni ule upachikaji wa viambishi kwa mzizi au shina na huweza kubadili kategoria ya neno lkn uambishaji ni pale viambishi vikipachikwa hubadili hali kama vile njeo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.