Je, ni kweli kwamba kuna kitu kinachoitwa Kiswahili Sanifu katika udhati wake, au hii ni dhana ya kitaalamu tu inayotumika kuelezea hali isiyokuwapo kwenye lugha, lakini mwa mantiki ya kuifanya ieleweke kwa jicho la wataalamu hao?
Je, kitendo cha ‘kusanifisha’ lugha ya Kiswahili kilikuwa cha kuja na kupita ama ni kitendo cha kuendelea, na hivyo hakikuishia kwenye miaka ya 1920 pale Mamlaka za Kikoloni katika Afrika ya Mashariki zilipoamua kuwa lahaja ya Kiunguja Mjini ndio uwe msingi wa Kiswahili Sanifu?
Na, suali kubwa kuliko yote, je chenyewe Kiunguja Mjini ndicho Kiswahili Sanifu? Suali hili pia linajirejea kwenye kinyume chake – je, Kiswahili Sanifu ni Kiunguja Mjini?
Una maoni gani? Tukisemee Kiswahili.
Zaidi tembelea ukurasa wa Kiswahili Kina Wenyewe wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle hapa.