Yatwawa nchi yatwawa, waichukua wenyewe
Yatwawa mbele kifuwa, kwa shangwe na kwa mayowe
Wenyewe waichukuwa, wainyakuwa ja mwewe
Na kwao yasubiriwa, yende ikapokelewe
Naiona yatwaliwa, ni wana vindakindaki
Benderaye yapepea, yendavye jitamalaki
Wako wanaochukiwa, hili wao hawataki
Ni lipi wataamua, watakuja watabaki?
Hamad Hamad
4 Machi 2014
Dodoma
Lau yatwawa itwawe, watawa wakiwa wao
Wakiwa ndiwo wenyewe, nchi yao watwaao
Naiwe hivyo naiwe, wasiwe ni wangineo
Watwae watwani wao, na wala wasizuwiwe.