Ya Rabbi nifungulia, milango yako nipite
N’ende unakokujua, siri na jahari zake
Lengo langu walijua, niauni nilipate
Ikiwa kuna ubaya, niepusha un’epuke
Kita’chokuwa cha kheri, kifupi ukirefushe
Kama kuwa ni kizuri, kigumu kilainishe
Kipe tamu ya sukari, kifanye kisinichoshe
Niwe nacho kwa dahari, moyoni kipendezeshe
Hamad Hamad
28 Januari 2014
Zanzibar