KISWAHILI KINA WENYEWE

Kuna Siku

Kuna siku nitalala, nilale nisiamke
Nilale bila khiyara, ulale muili wote
Iwe kama masikhara, nisifae kwa chochote
Sitakuwa miye tena

Siku hiyo nitaitwa, niitwe nisiitike
Mdomo taufumbata, alifu isinitoke
Nitakuwa nishasita, ‘shasita pumzi zote
Si mtu maana tena

Siku nitayotatafutwa, nitafutwe nisoneke
Ndotoni habaki otwa, hatamaniwa nituke
Nisituke haoneka, ibaki eepo kake
Dunia si pangu tena

Hamad Hamad
28 Machi 2013
Pemba

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.