Chawa sasa huna budi , uniondoke kichwani
Uwe na mimi baidi, japo kuwa umachoni
Nafanya hivi kusudi, kunusuru langu ini
Chawa uuke kichwani ijapo umeshitadi
Kweli wenitia hamu, wakati nilikinywani
Nekuwa mwendawazimu, hijiona namba wani,
Kumbe waninyonya damu, sasa nimeshabaini
Chawa uuke kichwani, wakati usalazimu
Niiona fahari, chawa kweli siutani,
Ela nazidi kariri, niache nitaabani
Tena ‘sifanye kiburi, kwamba wekubaliani.
Nataka utamakani, jambo hili le hiari
Wakati siwako tena, nakuonea imani
Huna tena la kunena, likangia sikioni
Uka dunia ni pana, kwengine ukazaini
Chawa uuke kicheani, sikuyo imewadia
Said O. Shoka
Zanzibar