Ni vitungwa aombaye, asijuwe kataliwa
Afukuzwae kwa mawe, bado akan’gan’gania
‘kakodowa mijichoye, huruma kutarajia
Akarehani utuwe, heshimaye kuivuwa?
Au ni kwa aombwaye, akakataa kutowa
Akaona abaniye, mkono kutofumbuwa
Hata asubukuliwe, katakata akataa
Asitake utamuwe, wengine kuuchukua?
Muombaji na muombwa, ni yupi kati ya hawa
Ni yupi ambae kwamba, mroho aweza kuwa
Nambiyani nawaomba, nipate kumtambuwa
Kati ya huyu na huyu, mroho hasa ni yupi?
Hamad Hamad
Copenhagen
25 Septemba 2012