Silipokuwa na shida, jumbale ejitolea
Jumba fakhari si haba, lote akanigaia
Simlipe hata haba, ya jazaa ekataa
Akanamba nihamiye
Thumma nikajwa na shida, sindano ya kushonea
Bilaye uchi ‘tenenda, n’adhirike na dunia
Kwa udhu henda muomba, adhara haambulia
Ya kuambwa niawiya
Hamad Hamad
Copenhagen
8 Septemba 2012