Mfanowe sijaona, kikombecho duniani
Chenye heba ya maana, na shepu ya wastani
Katu hakijafanana, na chochote kwa uzani
Kina marembo ya shani, na umbo lilotonona
Mitumko ya pembeni, tumtum imetuna
Na makiye ukingoni, burda metulizana
Kikishikwa chashikana, chatulia mkononi
Hakipwayi chajibana, kikajaa kiganjani
Sitaki kisifu sana, haja kitoa thamani
Kidole kimebaini, raha inopatikana
Kingiapo mkononi, mwa kikombe kikazama
Kikenda juu na chini, mdomoni kwa kupima
Kikombe nnokisema, si cha kahawa jamani
Sicho mnachokiona, kwa macho yenu ‘tamani
Ni kikombe nnochona, kwa jicho la hisiani
Hamad Hamad
Copenhagen
06-09-2012
kake chanimaliza hicho kikombe….! sababu cjapata ona mwangu maishani