Laiti kilio hiki, kinge cha hudhuni na masikitiko
Kuwa hunitaki, mwako himayani kuwa mwenza wako
Nami nge’ na dhiki, za umaskini sina penginepo
Lau ungekuwa mwema, ningelikuganda hakupembejea
Singekuwa mkhiyana, ningelikupenda na kukuridhia
Ela hilo huna, penzi lishavunda lajibomokea
Nalia hicheka, kwamba sasa basi tushamalizana
Kwa tushapofika, hutanishawishi hatizama nyuma
Miye nachomoka, ndio ma’alesh kabadili jina
Hamad Hamad
Copenhagen
19 Aprili 2012