Kiswahili kina ladha yake. Hapana shaka ni lugha zote, ingawa kwetu hili ndilo titi la mama, halishi hamu. Kitenzi ‘piga’ kinaweza kuonekana kuwa na maana mbaya katika hali yake ya awali, maana humaanisha ‘shambulia’, ‘dhuru’, ‘umiza’ na mengine yenye mshindo kama huo.
Lakini kwa ladha yake ilivyo njema, Kiswahili hukitumia kitenzi hiki kujengea vitenzi vyengine kadhaa vyenye maana tafauti kabisa na asili ya neno ‘piga’. Kwa mfano, ‘piga simu’, ‘piga soga’, ‘piga mbizi’, ‘piga moyo konde’, na mengineyo mengi.
Hebu nipe mifano zaidi uijuayo ya kitenzi ‘piga’ kiongezwapo na nomino.
piga gumzo, piga pasi, piga foleni, piga msitari
Ahsante Mwalimu Omar Babu