KISWAHILI KINA WENYEWE

Ubantu na Uarabu wa Vivumishi

Kivumishi ni aina ya maneno inayoliezea jina. Kuna vivumishi vya aina nyingi, ikiwa tunakusudia kuvigawa kwa makundi. Lakini muda mchache nilionao leo, nitautumia kuzungumzia aina mbili kati ya hizo – vivumishi vya idadi na vya sifa.

Katika aina zote mbili, kanuni moja inatawala. Nayo ni kuwa yale vivumishi vyote vyenye asili ya lugha za Kibantu vinachukuwa viambishi awali vya jina linalokielezea, ambapo vile vyote ambavyo vina asili ya lugha za Kiarabu, havibebi viambishi hivyo.

Katika vivumishi vya idadi, nambari zinazochukuwa viambishi vya majina ni zile za Kibantu: moja, mbili, tatu, nne, tano, na nane; na sio sufuri, sita, saba na tisa. Kwa mfano, tunasema: “Watoto watano” na au “Watoto sita” na sio “watoto tano” au “watoto wasita”.

Hali iko sawa kwenye vivumishi vya sifa. Vivumishi vyenye asili ya Kibantu kama vile -refu, -embamba, -zuri na -kubwa, huchukuwa viambishi awali vya majina vinavyoyaelezea. Lakini vivumishi kama rahisi, madhubuti, dhaifu na kamili havichukui viambishi awali vya majina vinavyoyaelezea.

Kwa mfano, tunasema: “Kisu changu ni kifupi lakini madhubuti”, sio Kisu changu fupi lakini kimadhubuti.

Mwisho, tuzungimzie vivumishi vinavyoelezea rangi. Hapa pana tafauti kidogo, kwani mstari uliopo baina ya vivumishi vipi viwekwe viambishi awali vya majina na vipi visiwekwe, hauna uhusiano na asili ya kivumishi kinachohusika. Kwa mfano, rangi kama -eupe, -eusi, -ekundu huchukuwa kiambishi cha jina, lakini vivumishi kama buluu, kijani na manjano havichuki sura hiyo.

Hapo patoshe kwa leo.

2 thoughts on “Ubantu na Uarabu wa Vivumishi”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.