KISWAHILI KINA WENYEWE

Herufi na Sauti za Kiswahili

Kiswahili kilipoanza kurikodiwa kimaandishi hakikuwa kikiandikwa kwa herufi hizi zinazoitwa za Kilatini, bali kwa zile za Kiarabu. Kwa mtazamo wangu, miongoni mwa misiba mikuu iliyokikumba Kiswahili ni huu wa kubadilishwa herufi zake mwanzoni mwa karne ya 19 baada ya upwa wa Afrika Mashariki kuvamiwa na Wazungu wakoloni.

Waliokiweka kwenye rikodi wakafanya hivyo wakizingatia kanuni na miundo ya lugha za Kizungu na kupuuzia ukweli kuwa Kiswahili si Kizungu wala hakikaribiani kabisa na lugha za Ulaya. Kidogo kidogo Kiswahili kikaanza kupoteza na miongoni mwa yaliyopotea pamoja na maandishi yake ya asili, ni matamshi yake.

Leo hii ukiuliza herufi za Kiswahili, basi utatajiwa zile za Kizungu, kasoro ya X. Ukiuliza irabu, nazo pia ni hizo hizo – a, e, i, o, u. Ni kama vile Kiswahili ni tawi miongoni mwa matawi ya lugha za Kizungu. Kumbe hivyo sivyo ilivyo. Kiswahili ni Kiswahili – Kibantu kwa sarufi yake, Kiarabu kwa msamiati wake. Ukweli huo ndio unaoakisika katika maneno, matamshi, sauti na miundo yake.

Leo hii, kwa sababu ya kulazimisha kukitenga Kiswahili na asili yake, kuna herufi zinazowakilisha sauti za Kiswahili zinafutwa kwa makusudi. Sauti kama gh, kh, tw, hh, th, na dh sasa zinapigwa vita. Lile lengo la kuifanya herufi kuwakilisha sauti za kwenye lugha linapotoshwa.

Wanaofanya hivyo wanajenga hoja yao juu ya Ubantu wa Kiswahili na wanashindana na uhalisia kuwa Kiswahili si Kibantu pekee.

4 thoughts on “Herufi na Sauti za Kiswahili”

  1. Mm kwa upande wangu nataka nizungumzie hapo uliposema kuwa kiswahili ni kibantu kwa sarufi yake na ni kiarabu kwa msamiati wake.Katika kipengele hichi ulichosema kuwa kiswahili ni kiarabu kutokana na msamiati wake ninakuwa na mtazamo tofauti. Kwani mimi naweza kusema kuwa kiswahili ni kiarabu kwa jina lake na si msamiati wake.Nathubutu kusema hivi kwani hili jina la kiswahili linatokana na waarabu ambao walikuja ktk upwa wa Afrika ya mashariki na wakawakuta watu wa upwa wa Afrika ya mashariki na wakawaita wasahel.Pwani yenyewe ikaitwa Sahel na kwa hivyo lugha ya watu wa pwani ikaitwa kisahel ambacho ndicho hichi kiswahili cha leo. kwa upande wa msamiati nadhani hoja yako ya msingi imeegemea zaidi kwenye msamiati wa kiarabu kwenye kiswahili. Sasa hapa unapoangalia hata huo msamiati wa kiarabu utakuta kuwa ni asilimia 31 wakati lugha za kibantu zimechangia asilimia64’pamoja na lugha nyengine kama vile kihindi,kireno,kijerumani zimechangia asilimia 5 tu. Vile vile hata huo msamiati wa kiarabu kuingia ktk kiswahili basi hiyo ni tabia ya lugha kuweza kuchukuliana maneno.Kwa hivyo nahitimisha kwa kusema kuwa kiswahili ni kiarabu kwa jina lake na naona si msamiati wake, au unaonaje juu ya hilo?.

  2. Nakushukuru Khelef kwa mchango wako. Nimeifahamu hoja yako, kuwa Uarabu wa Kiswahili kama upo, basi upo kwenye hilo jina tu. Hoja yangu inakwenda mbali zaidi. Inasema kwamba Uarabu huo upo, na upo kwenye msamiati wa Kiswahili kama lugha na si kama jina. Si kweli kwamba ni asilimia 31 tu ya maneno ya Kiswahili yanatoka kwenye Kiarabu. Utafiti nilionao mimi kutoka kwa Hassan al-Jabri ambaye alikuwa mwanafunzi wa PhD katika Chuo Kikuu cha Khartoum, ni kwamba ni asilimia 57 ya maneno ya Kiswahili yenye asili ya Kiarabu. Mengine ni maneno ambayo hata usingeliyafikiria kama vile dirisha, shaba na kofia. Utafiti huo nikiujumlisha kwenye uzoefu wangu binafsi kama mzawa wa Kiswahili, unanipa nguvu ya kusimama na kusema: “Kiswahili ni Kiarabu kwa msamiati wake na Kibantu kwa sarufi yake!”

  3. ulipoandika herufi,silabi na sauti nilitarajia kuona hizo herufi kwa mapana, sauti na silabi cha kushangaza hakuna kabisa mambo hayo nashindwa kuelewa ulikusudia nini kwa kichwa cha habari ulichoandika!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.