Nawaje na siye twenda, twenda haturudi nyuma
Waje wajavyo mafamba, katu hatutasimama
Tutenda tushajipanga, woga hatunao tena
Tutenda tukapambane
Wabofya hapabofyeka, papagumu amba chuma
Zama mpya zishafika, zama za kutuniana
Waje kwa mindu na shoka, kwa yiyo tutawanama
Wantuanza, tuwane
Nyuki ishalengwa ndimu, sasa hapebu kalika
Ng’ombe kakata ujamu, uhuruwe autaka
Na siye tumahajumu, kisasi twataka lipa
Pamoja tutasimama
Hamad Hamad
19 Januari 2012
Copenhagen