KISWAHILI KINA WENYEWE

Kulazimisha Umoja na Wingi

Kama zilivyo lugha nyengine, Kiswahili nacho kina majina mengi yasiyo Umoja au yasiyo Wingi. Nakusudia si kila jina (nomino) lina umoja au wingi. Yako mengi yenye kimoja kati yao. Watumiaji wa lugha ya Kiswahili wasio Waswahili wanapatishwa tabu na ukweli huu.

Katika uzoefu wangu wa ualimu wa lugha na uandishi wa habari, nimekutana sana na kadhia hii. Hapa nitatoa mifano michache. Katika habari huwasikia waandishi wenzangu wakisema ‘shambulizi’ wakitafsiri neno ‘attack’ la Kiingereza. Lakini kama lilivyo neno ‘matumizi’, neno ‘mashambulizi’ nalo pia  halina umoja kwenye Kiswahili hata kama lina umoja na wingi kwenye lugha nyengine. Hatusemi ‘tumizi langu la pesa limezidi uwezo’ hata kama tumetumia mara moja tu. Basi ndivyo pia ilivyo kwa ‘mashambulizi’.

Maneno mengine mfano wa hili ninayokuta yakilazimishwa yawe na umoja ni kama vile ‘mahitaji’ kwa kusemwa ‘hitaji’, ‘madhumuni’ linalosemwa ‘dhumuni’ na ‘matarajio’ linalolazimishwa liwe ‘tarajio’. Utasikia, kwa mfano, ‘Tarajio la Umoja wa Mataifa ni kumalizika haraka kwa mauaji nchini Syria.’

Nifupishe hapo kwa sasa.

2 thoughts on “Kulazimisha Umoja na Wingi”

  1. Hii ndio tatizo ya kutokuwa na madaraka na lugha wale wenye lugha sasa hivi waswahili sio wenye kuisarif luhga yao,watu ambao kiswahili ni lugha yao ya pili au hata inaweza kuwa ni ya tatu ndio wenye madaraka na kiswahili na hutaka lazima ilingane na lugha zao kama vile lugha hizi zina msamiati mmoja na tatizo jingine kutokana na upungufu wao wa msamiati hubuni au hutoa maneno kutoka lugha zao na kututilia katika kiswahili kwa kisingizio kuwa hakuna maneno ya kiswahili kumbe niuchache wao wa msamiati wa lahaja zingine za waswahili hawazijui.turudi katika mada inoyohusika ya maneno yenye umoja au wingi,sieahamu kwanini neno lenye asili au mtizamo wa umoja hutumika kwa wingi bila ya matatizo mfano bahari ikiwa moja au zaidi haziwi mabahari lakini neno lenye mtizamo wa wingi mfamo madhhebu likikiwa ni moja huliita dhehebu ,neno madhhebu sio neno wingi au umoja asili yake kwa upungufu wakufhamu hil neno asili yake wameoma kwasabu limeanzia na MA basindio wingi.sasmazungumzo itakuwa vp ,na ikiwa gumzo au porojo.lazima kiswahili kiwachiwe waswahili wenyewe.

    1. Ahsante Changuu kwa mchango wako. Ni kweli, neno madhehebu halina umoja. Ni kama ilivyo kwa maji, mapenzi, mazungumzo na mengi ya mfano na muundo huu. Siku nyingi tuliwaachia hawa lugha isiyokuwa yao kujifaragua nayo. Sasa Tuchukuwe hatamu wenyewe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.