KISWAHILI KINA WENYEWE

Vitenzi Vitano vya Kiswahili

Kama ilivyo kwa lugha nyengine, Kiswahili pia kina aina za maneno ambazo huwa zinakengeuka kawaida za maneno mengine kwenye lugha. Kwa mfano katika kundi la vitenzi, kuna vitenzi hivi vitano: kula, kunywa, kufa, kunya na kwenda.

Vitenzi hivi vina silabi mbili katika muundo wake wa msingi na hivyo mzizi wake huwa ni silabi au herufi moja tu. Kitenzi ‘kula’, kwa mfano, mzizi wake ni herufi ‘l’ tu, ambapo kitenzi ‘kunywa’, mzizi wake ni ‘nyw’.

Vitenzi vyengine vya kawaida kwenye Kiswahili, huwa na silabi zaidi ya mbili, yaani huanzia vitatu kwenda juu. Vitenzi ‘ kusema’, ‘kutembea’, kukimbilia, ni baadhi ya mifano ya vitenzi hivyo. Mzizi wa vitenzi kama hivi huanzia na silabi mbili au zaidi. Mzizi wa kitenzi ‘ kusema’, kwa mfano, ni ‘sema’, wa ‘kutembea’ ni ‘tembea’.

Kwa mzungumzaji wa kawaida na ambaye Kiswahili ni lugha yake ya kwanza, huenda hata asizingatie kuwa lugha yake ina tafauti hii, maana amekulia akiyatumia maneno hayo kama yalivyo. Tatizo liko kwa mgeni ambaye Kiswahili ni lugha ya kujifunza ukubwani. Ndipo unaposikia mtu huyo anasema ‘ukule’ kwa maana ya ‘ule’.

7 thoughts on “Vitenzi Vitano vya Kiswahili”

    1. Mzizi wa kitenzi kusema ni ‘sem-‘, ikiwa ‘sema’ inakuwa tayari imeshaongezewa kipashio mwishoni (kiambishi tamati) mwa mzizi na hivyo kuifanya kuwa kitenzi cha kuamrisha mtu mmoja.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.