Nakupenda, Zanzibar nchi yangu
Nitakulinda, kwazo zote nguvu zangu
Sitokwenda, kokote kwa mwezangu
Nitakuganda, hadi pale tamati yangu
Khelef Nassor Riyamy
27 Disemba 2011
Pemba
Mwana zidi kuipenda, nchi yako ya uzawa
Siku mbali ukenenda, kwa sababu itokuwa
Uivae kwenye chanda, ‘siache ikatwaliwa
Na tayari uwe wawa, siku zote kuilinda
Mohammed Khelef Ghassany
27 Disemba 2011
Bonn