Kila kitu duniani hutazamwa asiliye
Tonge hugwa mkononi ikaanguka wenyewe
Na hali waitamani mdomoni isingiye
Ikakutia tufani na katu isirejee
Khelef Nassor Riyamy
28 Disemba 2011
Pemba
La kudura mpwa wangu, lina Muungu pekeye
Ndiye mpanga mafungu, na riziki agawaye
Uloyanena mwanangu, kubwa mno maanaye
Allah ndiye atowaye!
Mohammed Khelef Ghassany
29 Disemba 2011
Bonn