Ni mpweke maishani, sina wa kuniokoa
Ni mpweke ni tabuni, hakuna anayenijua
Ni mpweke nikizani, hapana wa kunondoa
Ni mpweke nidhikini, ndugu wananihadaa
Ni mpweke mashakani, hekuna wa kunitoa
Ni mpweke ni ndiani, siji kwa kuelekea
Ni mpweke adhabuni, sina wa kusaidia
Ni mpweke Athumani, baba ameshajifia
Ni mpweke hadi lini, tabu ‘taniondokea?
Ni mpweke ghadhabuni, sina pa kutulizia
Ni mpweke ni motoni, sijui wa kun‘opoa!
Ni mpweke!!
Othman Ali Haji,
25/11/2011,
Zanzibar