Zama Mauti nifika, nikaitwa na Rabbuka, papo hajifia,
Zamu yangu imefika, Kaburini nikizikwa, nanyi mkinifukia,
Mkimaliza mwauka, mwaniacha weweseka, kwa upweke lonachia,
Habakia milenia, Dua njema kwimbiwa!
Zeraili kinijia, roho yangu jitwalia, namimi papo heliya,
Nakumbuka swahibia, dunia lowaachia, na wao wefurahiya,
Najua nenda mkiwa, sena wa kunifatia, nikawa nae pamoya,
Kwavyo newa Masikini!
Siku watu wanizika, kesha wenda pumzika, keniacha mpwekeya,
Kiifikiri nayuta, matendo ovu futika, na dhuluma itendeya,
“Ngeweza ngeimarika, akhera nikiishika, kiighiriki duniya”
Mayuto kila hayuta, Hakuna nosaidia!
Siku hiyo ni nzito, wafungwa kama kipeto, watupwa kijachiliya,
Wageuka ni mtoto, waliya bila kipato, hakuna we kuombeya,
Msaada ulonacho, saidizi wa mkato, matendo mema tendeya,
Naiogopa Milele, siku hiyo ifikapo!
Kwangu mwana Ali Haji, kujinusuru khitaji, mema nikijitendeya,
Dhuluma nisikhitaji, maovu siwe mtaji, kwayo nikajilemaya,
Nirejele kwa Mumbaji, msamaha nitaraji, huenda tasameheya,
Nijiandalie sasa, maisha ya Milenia!!!!!
By,
Othman Ali Haji,
20/11/2011,
Zanzibar.