Nipa moyowo ningie, ningie nizame ndani
Nitamakani nipoe, nilewe mwako penzini
Penzinimwo niwe miye, ndiye peke maishani
Nipa sitakuumiza, nipa nitakutunzia
Nifungulia nipite, ndani unikomelee
Watamanio wasite, karibu wasisogee
Watwone waawe mate, siri yetu wasijue
Nipa sitakuumiza, nipa nitakutunzia
Nifungia ndani yawo, uwe ndio ngome yangu
Nifanya mahabusuwo, nitia humo na pingu
Ukinifanyia hayo, sitakulipa machungu
Nipa wala usikhofu, nipa ‘tauengaenga
Hamad Hamad
22 Oktoba 2011
Oslo