Seraduwa numonumo, le vizo la kuvizizwa
Nevizwa kimapambano, hafikizwa tamauzwa
Tamaa gonga ukomo, hakwamwa, hakimbilizwa
Ndipo hafikia pano
Dahari numonumoni, nimo nikinumanuma
Nasonga nenda usoni, kina hikichunza nyuma
Sebu ubwaga watwani, kwawo peke najivuna
Ndivo haoneka vino
Wanamba sasa wanebu, hasukume gurudumu
Ela nacha kujaribu, haja hagwa nisiqimu
Hilo nalicha ajabu, nalo lanitia gamu
Kwanza mie poo simo
Hamad Hamad
Dubai
September 08, 2011