Kake njo’vyo nyumbani, uje uone rahaye
Uje wende forodhani, na shamba utembeleye
Usikie waadhini, mbio uwakimbiliye
Bi mama akutamani, na wana usikisiye
Njoo kake njoo, njoo ututembeleye
Nakwita uje nyumbani, upate ya kuandika
Ya mengi tele pomoni, mazuri na ya kunuka
Ya siasa na ya dini, ya ndoa na ya talaka
Ya kujuana ubini, na kupana madaraka
Njoo uyandike pya, kake uyandike yote!
Hamad Hamad
26 Juni 2011
Zanzibar