Nayacha macho ya wachwa, pale zama yachunzapo
Nayacha kucha na kuchwa, yachecheapo nilipo
Nayo yakijua yachwa, ndo uchunzi uzidipo
Nacha sitachapo kucha, yachwayo nami nayacha
Nacha wachwao na wacha, nawacha mana wachisha
Wasichwapo na wanapochwa, s’achi kuwacha nawacha
Na wachaji nasi twachwa, tusinacho cha kutisha
Nacha sitachapo kucha, pachwapo nami napacha
Nacha kwombwa ns’onacho, chacha kikanichachisha
Kyombwacho kifichoficho, chachisha na chashakisha
Nisichokimilikicho, chocho si changu nakicha
Nacha sitachapo kucha, kichwacho nami nakicha
Hamad Hamad
26 Mei 2011
Copenhagen
Simche msicha nchi, asiyewacha watuwe
‘Siyewacha wananchi, msaliti wataniwe
Hachiki huyu simchi, nataka ‘simche nawe