KISWAHILI KINA WENYEWE

Siku ya Furaha

Siku ikifika, tajifunga lemba
Nipite hicheka, kina hijigamba
Furaha hakika, itavunja myamba
Siku ya furaha

Siku hiyo hasa, ndio siku yangu
Ya kusema sasa, nami mlimwengu
Zama zimekwsiha, kumeza machungu
Siku ya furaha

Tapiga miluzi, nyote musikiye
Mupate maizi, furaha siriye
Munipe pongezi, munikumbatiye
Siku ya furaha

Siku naingoja, na yakaribiya
Siku ya faraja, ya kusherekeya
Sitaki itaja, ‘taniharibiya
Siku ya furaha

Hamad Hamad
7 Mei 2011
Copenhagen

3 thoughts on “Siku ya Furaha”

 1. siku hiyo ikifika, kake siache nambia
  siku hiyo ya baraka, kweli inakaribia
  jitayarishe kudaka, la kwangu takupatia
  sote tutafurahika, ewe mola jaalia

 2. siku hiyo babake, nami tafurahia
  tatamba kwa makeke, wote tajionea
  tamrushi mateke, yule ataejinamia
  nami tafurahia, ewe mola jaalia

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.