Mke mithili ya shamba, anahitaji matunzo
Msiishi kama samba, mwisho hata hapa mwanzo
Muijenge yenu nyumba, kwa kuyafata mafunzo
Ndoa Mola twamuomba, iwe ni cha kheri chanzo
Akikosa mwanamke, ‘simshikie upanga
Si magumi na mateke, mke hupigwa kwa kanga
Mwanamke mbavu zake, kila siku bado changa
Ukizinyosha kwa nguvu, ni bure utazivunja
Seyph Njugu
03.05.2011
Zanzibar