Vipi wajipaparisha, umoja ‘meukhalifu
Zama zake zimekwisha, upo kundini mwa wafu
Sasa ni kubahatisha, shuruti pazuke tifu
Kwa nini mwalazimisha? Muungano umekwisha
Watu mlibabaisha, mkajipa uzoefu
Watu mkawatingisha, nyoyo ziwajae khofu
Nishani mkajivisha, kujifanya watukufu
Kumbe mkitugeresha, Muungano ni dhaifu!
Seyph Njugu,
03.05.2011
Zanzibar