Mimi nawapa hongera, tena hongereni sana
Mumefanya ya busara, matendo ya kiungwana
Tukisimama imara, mambo yetu yatafana
Zanzibar ni yetu sote
Zanzibar ni yetu sote, lazima kuitetea
Tukiiacha itote, wenyewe tutaumia
Tukisimama kidete, nani atatuchezea?
Huu wajibu kwa wote
Huu wajibu kwa wote, ya mgambo imelia
Pale ulipo popote, ya mgambo imelia
Tumia nguvu yeyote, mawazo au rupia
Tupate Zanzibar yetu
Bin Hakum,
27 Aprili 2011