Hata akivua gamba, sumu yake bado kali
Nyoka huyu ndiye mwamba, kuteka zetu akili
Ameshiba na kuvimba, kwa zetu rasilimali
Kifo chake nakiimba, tayari kalala chali
Abuu Ahmad Al-Nofly
17 Aprili 2011
Joka la mdimu joka, mdimuni makaziye
Si zake ndimu hakika, ni zetu siye wenyewe
Hata tukitaka pika, hataki tuzitumiye
Kifoche kishamfika, azikwe na migambaye
Hamad Hamad
17 Aprili 2011
Huyu si wa kumzika, heshima hastahili
Mwenye nyoka kaondoka, chatula chake kivuli
Kifo chake kimefika, sumuye haihimili
Wa kufukiwa hakika, tusahaulie mbali
Abuu Ahmad Al-Nofly
17 Aprili 2011