Mola wetu mtukufu
Mola wetu maarufu
Nchi yetu i dhaifu
Twaja kwako tukilia
Twaja kwako watukutu
Mafakiri tuso kitu
Tupokee Mola wetu
Pa kutuweka wajua
Yaondoshe majeraha
Na fadhaa na karaha
Thamma utupe na jaha
Utuongoze na njia
Uzidi wetu umuri
Na kila jambo la kheri
Tuondoshee ya shari
Mbele ilotukalia
Tunusuru waja wako
Kwa vioja na vituko
Ili tukae kitako
Na nyoyo kututulia
Seyph Njugu
25 Aprili 2011
Zanzibar