Hamad Hamad Machi 10, 2011 Copenhagen
Sichami ago hanyela, nacha kuja wiya papo
Senda mbali hazurura, hasahau niwiyako
Taenzi ago kabula, sijafikwa ni mafiko
Tatukanaje wavyele, na uzazi ungalipo?
Sitacha m’bacha wangu, kwa mswala wa kupita
Habeza na walo wangu, waloniendesha tata
Wao ndio myega yangu, myengine sitaipata
Nshafunzwa n’mamangu, ‘limwengu haunipata
Mohammed Ghassany; Machi 10, 2011 Bonn
Ndiyo fakhari ya kwao, kucha kulichama ago
Ajuwaye lilo lao, halachi lingawa zigo
Palipo pao ni pao, pangakuwa penye gogo
‘Tayachamaje magua, na machumi yangalipo?
‘Sichame ndia ya kwenu, kuno iliyokuleta
Yewa mabuma mananu, yakapita ya kupita
Kidungu, michi na vinu, na mitwango na kupeta
Ndimo tulimokulia, akhi yangu ndimo mwetu
Ni mtumwa msi kwao, na ugeni ni madhila
Waulize watangao, waso chago ya kulala
Miye nawe sio hao, sifa kwa Mola Taala
Tuna kwetu, kwetu hasa, twitako tukaitikwa!