Kiti kye miliki yangu, yukaja dhalimu
Yukaniondosha
Yukaiba hadhi yangu, na pya majukumu
Yukanivulisha
Kwa nguvu za walimwengu, na sauti ya kalamu
Yukajikalisha
Yukitumilia
Kiti kye na maguu mane, yukakihujumu
Kunidhalilisha
Yukataka yusimame, kwa yake isimu
Yangu kufutisha
Ndipo yukafanya shime, na yake kaumu
Yukajisimisha
Yukin’gan’gania
Kiti kye uthibitisho, wa wangu uhuru
Kuuhalalisha
Kye ni kitambulisho, kwa walio huru
Hijitambulisha
Changu tena sicho, kashanikusuru
Chini nakalishwa
Hebu kiachia
© Hamad Hamad
April 2, 2011
Geneva