Hutwaa mizani, kupima utukufuwo
Hwenda chini, mno sana upandeo
Ile ya thineni, yenye tele mashindio
Haiji chini, ni mkubwa uzitowo
Mi’ sipaoni, ushudupo mfanowo
Nife leo ama kesho, ndanimo nanichimbiwe ufuwo!
Mohammed K. Ghassani kutoka Diwani ya Kalamu ya Mapinduzi