Mohammed Khelef Ghassani
Meine Damen und Herren,
Seit sieben Jahren arbeite ich mit der Deutsch-Tansanischen Partnerschaft e.V als Kisuaheli Lehrer für Freiwellige die nach Tansania kommen. Zwei mal bin ich schon in Deutschland bei der DTP gewesen.
Als Kisuahelilehrer besteht meine Arbeit nicht nur darin die Sprache zu unterrichten, sondern die Kulturellentüren für diese Jugendlichen/jungen Menschen zu öffnen. Mit dieser Realität habe ich mehr gelernt als was ich unterrichtet habe. Es gibt immer neue Herausforderungen, Erkenntnisse, Überraschung und, natuerlich, Konfusion. Ein sehr aktueller Satz ist es Alles ist anders! Essen, Leben, Eigenschaften, Entwicklungen und natürlich unser Verständnis von der Zeit.
Zum Beispiel, Leute denken dass, wir in Sansibar Zeit ist gehört uns. Wir können machen was wir wollen, langsam und beschaulich. In Deutschland gehören die Leute der Zeit, das heißt die Zeit kontrolliert Leute und Leute sind aber nur Folgender der Zeit. Ich habe einmal eine Frage von mein Teilnehmer bekommen: ´Wieso begrüßen die Leute sich mit sehr vielen Wörtern in deiner Kultur?’ In meiner Muttersprache gibt’s mindestens fünf verschiedene Begrüßungen, alle mit langen Fragen und Antworten. Aber wir haben Zeit dafür.
In Sansibar rennen wir selten auf der Strasse. In Deutschland laufen Leute fast immer. Diese Eigenschaft hat auch unser Leben überzeugt. Aber vielleicht gibt es einen Grund dazu: in Sansibar ist es immer sehr heiß, man braucht nicht viel zu laufen, in Deutschland braucht man, weil es sehr kalt ist.
Trotz alle dieser Unterschiede, gibt’s auch sehr große Gemeinsamkeiten: unsere Menschheit. Deutscher oder Sansibarischer haben wir alle eine Hoffnung als Menschen. Wir haben aber einen einzigen Traum um für den wir leben. Wir wollen das Beste für unser Leben und unsere Zukunft machen.
Einmal waren ich und Andrea Karsten in Kisimkasi gewesen. Nach dem dieser Einheit habe ich einen Vers geschrieben:
Wie viele Wege soll ich folgen?
Wie viele um meine Ziele zu erreichen
Direkt gehe ich, keinen Halt da zwischen
Wenn du kennst, sag mal denn!
’Mohammed, ich weiß es gibt Wege, aber wie viele das kann ich nicht sagen. Das weiß ich nicht.’’ So sagte Andrea.
Wie ich, haben Andrea und das ganze Team von DTP auch ihren Weg gesucht. Sie haben einen Traum für den sie leben. Und dieser Traum war auch ihr Auftrag‚’’LICHT FÜR ALLE!’’ Am Anfang war es nur für ein kleines Dorf, Kisimkasi, im Suden Sansibar, aber heute ist es die Mission für das ganze Land, Tansania. Ein Licht von Solarenergie für alle. In letztem Monat war Sansibar in Dunkel weil etwas schlecht mit unseren Power-system passiert hat. Solarenergie Traum könnte dieses Dunkel weg machen!
Ich bin stolz dass ich ein Teil für diese heilige Mission bin. Ich helfe den Volunteers um ihr Ziel zu erreichen. Dessen suche und finde ich meinen eigenen Weg und darüber bin ich zufrieden und glücklich.
Ich danke Ihnen für Ihre Aufmerksamkeit
TAFSIRI ISIYO RASMI
Mafungamano ya Kitamaduni: Hisia za mtu tamaduni zinapokutana
Mabibi na Mabwana,
Kwa miaka saba sasa nimekuwa nikifanya kazi na Ushirikiano wa Ujerumani na Tanzania kama mwalimu wa Kiswahili kwa wanafunzi wanaojitolea kuja Tanzania. Mwara mbili nimeshawahi kuja hapa Ujerumani kwa ajili ya Jumuiya hii.
Nikiwa kama mwalimu wa Kiswahili, jukumu langu limekuwa sio tu ni kuwafunsiha lugha vijana hawa, bali pia kuwafungulia milango ya utamaduni wa jamii yangu. Na katika kutekeleza jukumu hilo, nimejikuta kuwa yale ninayojifunza kutoka kwa vijana hawa ni mengi na makubwa zaidi kuliko yale ninayowafundisha mimi. Daima kumekuwa na changamoto jipya, uelewa tafauti, mshangao na, bila ya shaka, mkanganyiko. Labda sentensi moja inayoweza kueleza hali hii ni kwamba “Kila kitu kiko tafauti!” Vyakula, maisha, tabia, maendeleo na, hapana shaka, ufahamu wetu kuhusu wakati.
Kwa mfano, watu wanafikiri kwamba sisi Wazanzibari wakati ni wetu, kwa maana ya kusema kwamba tunaweza kufanya kila tunalolitaka taratibu na pole pole, bila ya haraka. Tuna hata msemo kuwa haraka haina baraka. Hapa Ujerumani watu wamemilikiwa na wakati, kwa maana ya kwamba wakati ndio huwadhibiti watu na sio watu kuudhibti wakati. Mara moja niliulizwa swali na mwanafunzi wangu: “Kwa nini katika utamaduni wako watu hutumia maneno mengi kusalimiana tu?” Katika lugha yangu ya kuzaliwa, Kiswahili, tuna namna darzeni nzima ya kuamkiana na kila namna ina maswali na majibu marefu. Lakini tunao wakati wa kufanya hivyo, yaani kuulizana na kujibizana salamu.
Nyumbani Zanzibar, ni nadra kutukuta tunakwenda mbio barabarani. Hapa Ujerumani kila mara utawakuta watu wanakimbia barabarani. Tabia hii nayo inayaathiri maisha yetu, ingawa kila upande una sababu zake kwa hili: nyumbani Zanzibar mara nyingi huwa tuna hali ya hewa yenye joto, kwa hivyo mtu halazimiki kukimbia sana wakati wa kutembea, hapa Ujerumani mtu analazimika kutembea kwa kukimbia maana kuna baridi sana!
Hata hivyo, juu ya tafauti zote hizi, kuna pia jambo moja kubwa linalotuunganisha: nalo ni ubinaadamu wetu. Mjerumani ama Mzanzibari, sote tuna matumaini namatarajio kama wanaadamu. Sote tunaunganishwa na ndoto moja na ambayo kwayo tunaishi: tunataka kile kilicho bora zaidi kwa maisha yetu na kwa mustakabali wa vizazi vyetu.
Mara moja nilikuwa nipo na Andrea Karsten (kiongozi wa DTP) katika kijiji cha Kizimkazi. Baada ya kufikiria sana kuhusu jambo linalotuunganisha pamoja kama wanadamu, nikaandika beti chache za ushairi:
Njia ngapi nizandame, kunifisa nitakako?
Katikati nisikwame, nifike hima nendako
Lau weye wazijuwa, namba basi kama ziko!
“Kwa hakika, Mohammed, najua kuwa ziko njia, lakini ngapi, hilo siwezi kusema. Sijui!” Akasema Andrea.
Basi kama mimi, pia Andrea na timu nzima ya DTP wamekuwa wakitafuta njia zao. Wamekuwa na ndoto ambayo kwayo wanaishi. Na ndoto hii pia imekuwa ndio mwito wao: NURU KWA WOTE. Pale mwanzoni ndoto hii ilikuwa ni kwa ajili ya kijiji kidogo cha Kizimkazi, Kusini Unguja, tu, lakini leo misheni hii imekuwa kwa nchi nzima ya Tanzania. Nuru ya shati ya jua kwa watu wote. Katika mwezi uliopita, Zanzibar ilikuwa katika giza kwa takribani wiki nne kamili kwa kuwa mtambo wa kusafirishia umeme uliharibika. Ndoto ya nishati ya jua ingeliweza kulikimbiza mbali giza hili!
Basi leo ukiniuliza mimi ninajihisije, nitakujibu kwamba ninaona fakhari kuwa nimekuwa sehemu wa misheni hii. Ninawasaidia vijana kutimiza lengo lao na kwa namna hiyo hiyo nami natafuta na naiona njia yangu. Na kwalo, ninaridhika na nafurahi sana.
Nawashukuruni kwa usikivu wenu!
*Hotuba katika Maadhimisho ya Kumi ya Ushirikiano Baina ya Tanzania na Ujerumani (Deutsch-Tanzanische Partnershaft e.V), Altona Rathaus, Hamburg, Ujerumani, 5 Julai, 2008